Site logo
Quotex blog /Mkakati /Jinsi ya Kutengeneza Mkakati Wako Mwenyewe wa Biashara Hatua kwa Hatua
Mkakati

Oct 14

Jinsi ya Kutengeneza Mkakati Wako Mwenyewe wa Biashara Hatua kwa Hatua

Mkakati wa biashara si lazima uwe mgumu. Unachohitaji ni kuamua ni mali zipi ungependa kufanyia biashara, wakati wa kufungua na kufunga miamala, na kiwango cha hatari ambacho uko tayari kukubali. Baada ya hapo, unaweza kujaribu kanuni ulizoweka na kutathmini matokeo yake.

Ikiwa unataka kujua jinsi ya kutengeneza mkakati wako mwenyewe wa biashara, mwongozo huu wa hatua kwa hatua utakusaidia kuandaa mpango ulio wazi ambao unaweza kuujaribu kwa vitendo.

Hatua ya 1: Weka malengo yako na kiwango cha hatari unachoweza kukubali

Kabla ya kuchagua viashiria vya kiufundi au kutafuta ishara za kuingia sokoni, anza kwa kutathmini malengo na uwezo wako mwenyewe.

Jiulize maswali machache ya msingi:

  • Unataka kufikia nini kupitia biashara ya masoko ya fedha?
  • Unaweza kutenga muda gani kufuatilia na kuchambua soko?
  • Uko tayari kuhatarisha kiasi gani cha fedha?

Kwa mfano, mtu anayeweza kufuatilia chati kwa saa kadhaa kila siku anaweza kuhitaji mbinu tofauti na mtu ambaye ana dakika 20 pekee jioni.

Hatua ya 2: Chagua soko na kipindi cha muda

Hatua inayofuata ni kuamua ni mali zipi ungependa kufanyia biashara. Unaweza kuzingatia sarafu, hisa, bidhaa ghafi, fahirisi au vyombo vingine vya kifedha vinavyopatikana. Si lazima ufanye biashara katika masoko yote kwa wakati mmoja. Kuanza na soko moja kunaweza kukusaidia kuelewa vizuri zaidi jinsi bei zake zinavyobadilika kwa kawaida.

Baada ya hapo, chagua kipindi cha muda kinachofaa.

Kwa biashara za muda mfupi, unaweza kutumia chati za dakika moja au dakika tano. Kwa biashara zinazochukua muda mrefu zaidi, chati za kila saa au za kila siku zinaweza kufaa zaidi.

Ikiwa ndiyo kwanza unaanza kutengeneza mkakati wa biashara, ni vyema kuanza kwa njia rahisi. Chagua soko moja na kipindi kimoja au viwili vya muda. Jifunze jinsi bei zinavyobadilika kabla ya kuongeza zana na vigezo vingine.

Hatua ya 3: Weka kanuni za kufungua na kufunga miamala

Bainisha kwa usahihi hali ambazo zitakufanya ufungue au ufunge muamala.

Epuka kanuni zisizo wazi kama vile “Nitafungua muamala soko likionekana kuwa katika mwelekeo wa kupanda.” Kauli hii inategemea sana mtazamo binafsi. Wafanyabiashara wawili wanaweza kuangalia chati ileile na kufikia hitimisho tofauti kabisa.

Badala yake, weka masharti yaliyo wazi na mahususi. Kwa mfano, kanuni zako zinaweza kuwa:

  • Kufungua muamala wakati muundo fulani wa bei unapojitokeza
  • Kuthibitisha ishara kwa kutumia kiashiria cha kiufundi
  • Kutofungua muamala ikiwa hali ya soko haikidhi masharti uliyoweka
  • Kufunga muamala lengo lililowekwa linapofikiwa

Kanuni hizi za kufungua na kufunga miamala zinapaswa kuwa msingi wa mkakati wako wa biashara. Ni juu yako kuamua ni viashiria na ishara zipi utatumia. Jambo muhimu zaidi ni kujua hasa unachopaswa kuangalia kabla ya kufungua muamala.

Kanuni zilizo wazi pia hurahisisha kujaribu mkakati wako. Ikiwa unabadilisha maamuzi yako kila mara bei zinapobadilika, itakuwa vigumu kujua kama mkakati wako unafanya kazi kweli au kama ulipata matokeo mazuri kwa bahati tu.

Hatua ya 4: Weka kanuni za kudhibiti hatari

Pia unahitaji kupanga mapema utakachofanya ikiwa soko litaenda kinyume na utabiri wako.

Amua mapema kiasi cha fedha ambacho uko tayari kuhatarisha katika kila muamala na jinsi utakavyoshughulikia hasara zinazotokea mfululizo. Unaweza pia kuweka mipaka ya jumla kwa shughuli zako za biashara, kama vile idadi ya juu zaidi ya miamala au kiwango cha juu cha hasara kinachoruhusiwa katika kipindi kimoja cha biashara.

Kwa mfano, mpango wako unaweza kujumuisha kanuni zifuatazo:

  • Kuhatarisha kiasi cha fedha kilichowekwa mapema pekee katika kila muamala
  • Kutoongeza kiasi cha fedha katika muamala unaofuata kwa sababu tu muamala uliopita ulileta hasara
  • Kusitisha biashara unapofikia kiwango cha juu cha hasara ya kila siku ulichoweka
  • Kutofungua muamala kwa lengo la kufidia hasara za awali pekee

Kiasi husika cha fedha na mipaka inayofaa hutegemea hali yako binafsi na mkakati uliochagua.

Hatua ya 5: Jaribu mkakati wako kwenye akaunti ya majaribio

Usikimbilie kuanza kufanya biashara kwa kutumia fedha halisi. Kwanza, angalia jinsi mkakati wako unavyofanya kazi katika mazingira ya biashara ya majaribio.

Kwenye Quotex, unaweza kujaribu mkakati wako kwa kutumia akaunti ya majaribio. Akaunti hii ina fedha za majaribio na inakupa ufikiaji wa zana za biashara zinazopatikana kwenye jukwaa. Kwa njia hii, unaweza kufanya mazoezi, kutumia mkakati wako na kutathmini matokeo bila kuhatarisha fedha halisi.

Hatua ya 6: Tunza kumbukumbu za biashara na uchambue matokeo

Kumbukumbu za biashara zitakusaidia kuelewa vizuri zaidi sababu za kila uamuzi uliofanya na matokeo yaliyofuata.

Kwa kila muamala, unaweza kurekodi taarifa zifuatazo:

  • Tarehe na saa
  • Soko na kipindi cha muda
  • Viwango vya kufungua na kufunga muamala
  • Sababu ya kufungua muamala
  • Sababu ya kufunga muamala
  • Matokeo

Njia hii rahisi ya kutunza kumbukumbu za biashara inaweza kukusaidia kutambua mifumo inayojirudia ambayo huenda isiwe rahisi kuiona unapochambua kila muamala kivyake.

Huenda ukagundua kuwa mkakati wako unafanya kazi vizuri zaidi katika hali fulani za soko. Au unaweza kugundua kuwa mara nyingi unafungua miamala mapema mno. Inawezekana pia kwamba kanuni zako zinafaa, lakini unaendelea kuzipuuza baada ya muamala uliosababisha hasara.

Na kumbuka, kutengeneza mkakati wa biashara ni mchakato endelevu. Unaweka kanuni, unazijaribu, unakusanya taarifa, unachambua matokeo na kufanya marekebisho kwa uangalifu inapohitajika.

Imependekezwa